Kuhusu Mkopo wa Vikundi
Mikopo nafuu iliyobuniwa kusaidia vikundi na vyama vya kijamii. Kama wewe ni sehemu ya kikundi cha akiba, ushirika wa wanawake, vikundi vya maendeleo ya vijana, vyama vya biashara za kijamii, vikundi vingine vya ushirika, mkopo wa Vikundi itakusaidia kupata mtaji unaohitajika ili kukua pamoja na kufikia malengo ya pamoja.
Vigezo vya kupata mkopo wa vikundi
Kikundi kinatakiwa kuwa na watu si chini ya 5 na si zaidi ya 20
Kila mwanakikundi lazima awe na nakala ya kitambulisho
Kila mwanakikundi lazima awe na mdhamini
Kwa mwanakikundi aliyeoa au kuolewa lazima adhaminiwe na mume au mke wake
Kila mwanakikundi lazima adhaminiwe na wanakikundi wenzake
Kila mwanakikundi lazima awe na dhamana
Kila mwanakikundi lazima awe na kazi/biashara inayomuingizia kipato
Faida za Mkopo wa Vikundi
Uwajibikaji wa Pamoja
Riba ya Chini
Mkopo jumuishi
Wanachama wanasaidiana, jambo linaloongeza uwajibikaji na mafanikio ya urejeshaji wa mkopo.
Furahia masharti nafuu ya ulipaji yaliyobuniwa mahsusi kwa mikopo ya vikundi.
Unafaa hata kwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi, vikundi vya wanawake, na miradi ya vijana.
Wasiliana Nasi
-
Mwenge, Mkabala na Chuo Kikuu cha Tumaini
S.L.P 1234, Dar es Salaam, Tanzania -
+255 743 771 258
- info@upliftmicrofinance.co.tz
Kipeperushi
Tazama Kipeperushi kwa mwongozo rahisi wa kusoma kuhusu huduma zote tunazotoa.
